RUHAGOYACU.com

Singida United: Mshambuliaji Danny Usengimana kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja

Mshambuliaji wa timu ya Singida United ya Tanzania na timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) amepata matatizo ya kujeruhiwa mkono ambapo atabakia nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.

Usengimana amejeruhiwa katika mchezo na Mlandege FC katika michuano ya Mapinduzi Cup nchini Zanzibar baada ya kuandika bao la kwanza baadhi ya 3-0 ambayo Singida United iliichapa siku ya jana Ijumaa.

Akizungumza na gazeti hili leo, mshambuliaji huyo ametangaza kilichomkuta.

" Niliruka kwa kupiga mpira kwa kichwa huku nikajikuta nimeangukia mkono wangu na kuvunjika," Danny Usengimana amefafanua.

Katika ligi kuu, Usengimana ameshindia Singida United mabao 4 na katika michuano ya Mapinduzi Cup akashinda mabao 3 katika michezo 3.

Singida United watacheza na Yanga Africans Jumatatu kwa kutafuta timu itakayotinga nusu fainali ya mashindano ya Mapinduzi Cup.

Katika mashindano ya Mapinduzi Cup, Singida United wanaongoza kundi B na alama 12 huku Yanga Africans wakafuata na alama 9.

Map : Nyumbani  \  Afrika  \  Habari motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine