RUHAGOYACU.com

Breaking: Mgombea urais FERWAFA ashindwa kupata kura 27, Vincent De Gaulle Nzamwita aendelea kuongoza

Baada ya Vincent De Gaulle Nzamwita kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kusaka kiti cha urais Shirikisho la Soka Rwanda Ferwafa, naye mgombea urais pekee Bi Felicite Rwemalika ameshindwa kupata kura 27 ambazo angefaa kuzipata ili aibuke mshindi.

Katika uchaguzi huo, baadhi ya wapigaji kura 52, Bi Rwemalika amepata kura 13 na 39 nyinginezo zikawa bure.

JPEG - 89.5 kb
Bi Felicite Rwemalika ameshindwa kupata kura 27

Kiongozi wa tume ya uchaguzi Adolphe Kalisa ameambia vyombo vya habari kuwa kwa mujibu wa kipengele cha 28, uongozi wa zamani utabakia kushika usukani kwa muda wa siku 60 au 90 ambapo uchaguzi utakuwa unaendelea mpaka papatikane kiongozi wa shirikisho hilo.

JPEG - 78.7 kb
Ijapokuwa amejitoa kwa sababu zake binafsi, Vincet De Gaulle ataendelea kuongoza Ferwafa

Hapo, Vincent De Gaulle Nzamwita ataendelea kushika usukani ijapokuwa ametangaza kujitoa kwa sababu zake kibinafsi.

Map : Nyumbani  \  Baiskeli

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine