RUHAGOYACU.com

Louis Meintjes ateuliwa mwendesha baiskeli bora 2017 Afrika

Louis Meintjes ambaye anaichezea timu ya UAE Emirates ameteuliwa kama mwendesha baiskeli bora wa mwaka 2017 barani Afrika.

Tuzo hiyo imetolewa na waandalizi wa mashindano ya baiskeli La Tropicale Amissa Bongo.

Jopo la majaji kuamua mwendesha baiskeli bora liliongozwa na Bernard Hinault aliyenyakua mashindano ya Tour De France kwa mara tano, waendesha baiskeli machachari barani Afrika, makocha na viongozi wa mashirikisho ya mchezo huo.

Mnyarwanda Joseph Areruya anayeichezea Dimension Data Afrika Kusini amepata nafasi ya pili huku mwenzake Merhawi KUDUS akashika nafasi ya tatu.

Chanzo: Presse Release, La Tropicale Amissa Bongo

Map : Nyumbani  \  Baiskeli

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine