RUHAGOYACU.com

Samuel Mugisha aibuka kidedea wa hatua ya mwisho Rwanda Cycling Cup

Mwendesha baiskeli Samuel Mugisha anayechezea timu ya Dimension Data ameibuka kidedea hatua ya mwisho (Final Race) ya mashindano ya baiskeli ya Rwanda Cycling Cup baada ya kutumia muda wa saa 2 dakika 28 na sekunde 57.

JPEG - 110 kb
Samuel Mugisha akishangilia kuibuka kidedea wa hatua ya mwisho leo

Mpaka kumalizika, mashindano hayo yamechukua miezi tisa huku kwa ujumla timu ya Benediction ikitwaa taji la Rwanda Cycling Cup.

JPEG - 163.4 kb
Klabu ya Benediction ndio imetwaa taji la Rwanda Cycling Cup

Kuelekea hatua ya mwisho ya leo, waendesha baiskeli wamepambana wakitoka Gatuna mpaka jijini Kigali.

Hawa washindi watano wa hatua ya Final Race:
1. Samuel Mugisha (Dimension Data) 2h38’57”
2. Bonaventure Uwizeyimana (Benediction Club) 2h39’28”
3. Dukuzumuremyi (Fly CC) 2h39’28”
4. Rene Jean Paul Ukiniwabo (Les Amis Sportifs) 2h39’28”
5. Janvier Rugamba (Les Amis Sportifs) 2h39’28”

Map : Nyumbani  \  Baiskeli

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine