RUHAGOYACU.com

Wawakilishi wa Team Rwanda kushiriki mashindano ya baiskeli La Tropicale Amissa Bongo

Baada ya kufanya vema katika mashindano ya baiskeli ya Tour Du Rwanda 2017, nyota wa mchezo huo Valens Nsabimana na Areruya Joseph wanatarajiwa kuingoza Team Rwanda katika mashindano ya baiskeli ya La Tropicale Amissa Bongo.

Mashindano hayo yataanza kutimua vumbi mwaka ujao kuanzia tarehe 15 hadi 21 mwezi wa Januari.

Waendesha baiskeli wa Team Rwanda watapambana na wabingwa wa La Tropicale Amissa Bongo mfanowao Adrien Petit mwaka 2016 pamoja na Yohan Gene mwaka 2017.

Hawa wawakilishi wa Team Rwanda:
1. Joseph Areruya
2. Valens Ndayisenga
3. Bonaventure Uwizeyimana
4. Rene Jean Paul Ukiniwabo
5. Didier Munyaneza maarufu ‘Mbappe’
6. Jean Ruberwa

Hizi steji za La Tropicale Amissa Bongo 2018:
Januari 15 (Stage 1): Kango – Lambaréné, 146km
Januari 16 (Stage 2) : Ndendé – Fougamou, 173km
Januari 17 (Stage 3) : Fougamou – Lambaréné, 114km
Januari 18 (Stage 4): Ndjolé – Mitzic, 182km
Januari 19 (Stage 5) : Oyem – Ambam (Cameroon), 141km
Januari 20 (Stage 6): Bitam – Oyem, 115km
Januari 21 (Stage 7): Bikélé – Libreville, 140km

Map : Nyumbani  \  Baiskeli

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine