RUHAGOYACU.com

Wacheza Taekwondo wa Rwanda, Kenya na Uganda watia fora kwenye mashindano ya Korean Ambassador’s Cup

Kigali- Timu za Rwanda, Kenya pamoja na Uganda zinazojihusisha na mchezo wa Taekwondo zimefanya vizuri kwenye mashindano ya Korean Ambassador’s Cup ambayo yamefanyika mwishoni mwa wiki jijini Kigali.

Timu hizo zimefanikiwa kushindia medali mbali mbali.

Rwanda imeleta klabu kumi na nne ambazo zimeshindia jumla ya medali hamsini na saba kukiwa na medali za dhahabu ishirini na mbili.

JPEG - 146.5 kb
Rwanda ilitia fora kwenye mashindano ya Korean Ambassador’s Cup.

Miongoni mwa klabu ambazo zimewakilisha Rwanda, klabu ya Dream Taekwondo imetia fora kwa kuibuka na medali za dhahabu kumi na tatu.

JPEG - 148.2 kb
Wacheza Taekwondo wa kike wakipiagana.

Mwaka jana wa 2016, klabu hiyo tena iliibuka kidedea kwenye mapigano hayo ya mara ya nne yaliyotimua vumbi nchini Kenya.

Labda ushindi huo ndio umeihimiza Kenya kusaka medali mwaka huu wakileta hadi timu saba ambapo wamefanikiwa kupata jumla ya medali ya nane.

JPEG - 192.6 kb
Mashabiki wa mchezo wa Teakwondo wameongezeka nchini Rwanda.

Uganda imepata jumla ya medali kumi na nne, Kongo Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ikipata mbili, Sudani Kusini na Tanzania medali wakipata moja na Somalia kurudia nyumbani mikono wazi.

Kwa mara ya tano, mashindano hayo yameunganisha timu saba kutoka ukanda wa maziwa makuu.

Timu hizo ni Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania, Kongo Jamhuri ya Kidemokrasia, Sudani Kusini pamoja na Somalia.

Medali zilizozawadiwa washindi:
1. Rwanda: dhahabu 22 + fedha 14 + shaba 21 = 57
2. Uganda: 3 dhahabu + 7 fedha + 4 shaba = 14
3. Kenya: dhahabu 1+ 3 fedha + 4 shaba = 8
4. DRC: 1 fedha + 1 shaba = 2
5. South Soudan: 1 fedha
6. Tanzania: 1 shaba
7. Somalia: 0

Tuzo za wachezaji:
Mchezaji chipukizi bora wa kike (Best Junior female): Nadege Umurerwa (Rwanda)
Mchezaji chipukizi wa kiume (Best Junior male): Geofrey Gatari (Rwanda)
Mchezaj bora wa kike (Best senior female): Amina Namutosi (Uganda)
Mchezaji bora wa kiume (Best senior male): Benon Kayitare (Rwanda)
Kocha bora (Best Coach): Richard Kitol (Tanzania)
Refari bora (Best Referee): Emmnuel Musabyimana (Rwanda)
Fair-play Team: Shofco (Kenya)
Taekwondo Spirit): Somalia
Timu bingwa wa mashindano (Team champion): Dream Taekwondo Club
Taifa bingwa wa mashindano (Country Champion): Rwanda

Map : Nyumbani  \  Kwingineko  \  Taekwondo

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine