RUHAGOYACU.com

Wachezaji Wanyarwanda 13 wa timu ya Dream Taekwondo Club washindia medali nchini Kenya

Wachezaji 13 wa timu ya Dream Taekwondo Club kutoka Rwanda walishindia medali nchini Kenya kutoka mapambano ya kimataifa ya ‘Professors Cup International Open Championship’.

Tangu tarehe 23 mpaka 24 Julai mwaka huu, Dream Taekwondo Club wakuwa wanapambana na timu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda pamoja na Kenya.

Hii ilikuwa mara ya kwanza timu hiyo kushiriki mapambano ya kimataifa ijapokwa wachezaji walikuwa wanajawa na matumaini ya kuibuka washindi kulingana na mazoezi ya kiuweledi waliyoyapata awali.

Baadhi ya wachezaji 13, 9 walishindia medali za dhahabu na wanne wao za fedha wakachukua nafasi za pili katika makundi yao. Jumla ya medali hizo ilifanya Rwanda kuwa ya kwanza ikafuatiliwa na timu ya chuo cha Kibabi nchini Kenya.

Pia, katika timu ya Rwanda kulikuwa wachezaji vijana vipukizi chini ya umri wa miaka 16 watakaohudhuria kombe la dunia nchini Misri na michezo ya Olimpiki mwaka ujao.

Akizungumza na gazeti la RuhagoYacu, katibu mkuu wa shirika la Taekwondo Placide Bagabo alieleza kwamba vijana hao walishindia medali za dhahabu na wanaleta imani ya kuwa nguzo za kesho za mchezo huo na wakiungwa mkono watakuwa wa kutegemewa katika mashindano tofauti.

Mchezaji wa kike Aline Ndacyayisenga alichaguliwa mchezaji bora wa kike wa ukanda wa maziwa makuu ambapo alishindia medali ya dhahabu kwa wachezaji wenye uzito chini 53.

Ndacyayisenga alinyakua kombe hilo baada ya kuwa mchezaji bora katika mwezi wa Meyi katika shindano la Uganda Ambassador’s Cup.

Aliliambia gazeti la RuhagoYacu kwamba alikuwa tayari kabla kushiriki shindano pia alitia maanani kwamba alikuwa anapeperesha bendera ya nchi yake.

Eugene Ntawangundi kocha mkuu wa timu ya Dream Taekwondo Club alikabidhiwa tuzo la kocha mkuu bora wa shindano.

Map : Nyumbani  \  Kwingineko  \  Taekwondo

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine