RUHAGOYACU.com

Wawakilishi wa Rwanda watia fora kwenye mashindano ya Para-Taekwondo

Wawakilishi wa Rwanda wametia fora wakishindia medali mbalimbali kwenye mashindano ya Taekwondo ya welemavu (Para-Taekwondo) nchini Uingereza.

Ushindi huo ulipatikana jana Alhamisi Oktoba 19, 2017 ambapo mashindano hayo yalikuwa yanatokea jijini London, Copper Box, mbuga ya Malkia Elizabeth na kushirikisha wacheza taekwondo 263 kutoka nchi 59 ulimwenguni kote.

Kwa upande wa wanawake, mcheza taekwondo Consolee Rukundo alinyakua medali ya dhahabu wakati kwa wanaume Jean de la Croix Nikwigize aliye na ulemavu wa K41 alishindia medali ya shaba.

JPEG - 75.5 kb
Wacheza Taekwondo Consolee Rukundo kwa upande wa wasichama pamoja na Jean de la Croix Nikwigize kwa upande wa wavulana

Rwanda ilipeleka hapo wacheza teakwondo sita baadhi yao Jean Claude Niringiyimana alitangulia wenzake na kupiga Mkorea kwa alama 41-26 hivi mara ya pili akampiga tena Mrusi kwa alama 29-9.

Ushindi huo ulimpaisha kwenye kiwango cha dunia ambapo alipanda nafasi akitoka kwa nafasi ya kumi na tatu hadi ya tano kwa sasa.

Kueleka matokeo, Jean de la Croix Nikwigize alipata ushindi baadhi ya wachezaji wenye uzito chini ya kilo 61 wakati mwenzake Jean Marie Vianney Bizumuremyi alijeruhiwa na kujitoa katika duru ya robo fainali hivi Jean Pierre Manirakiza pamoja na Eliezer Tuyishime wakaondolewa mapema kwenye michuano ya makundi.

Kwa upande wa wanawake, Consolee Rukundo alishindia medali ya dhahabu katika kundi la wacheza Taekwondo wenye uzito chini ya kilo 58 wakiwa na ulemavu wa k42.

Map : Nyumbani  \  Kwingineko  \  Taekwondo

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine