RUHAGOYACU.com

Ghasia za uwanjani: Mchezo wa kirafiki wa Amavubi na Sudani wasimamishwa

Mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) na Sudani umesimamishwa kutoka na ghasia za wachezaji uwanjani.

Katika mchezo huo ambao umefanyika Sousse nchini Tunisia, kunako dakika ya 40 kipindi cha kwanza mchezaji wa Sudani Nasser Omar amefanyia kosa kiungo wa Amavubi Muhadjiri Hakizimana tena akampiga kichwa Yannick Mukunzi na makosa hayo yakamfanya mwamuzi kutoa free-kick kwa upande wa Amavubi.

Hapo, kipa wa Sudani Akram El Madii amewaongoza wenzake kuzua ghasia uwanjani na wachezaji wakaanza kupigana kisha mwamuzi akasimamisha mchezo.

Mchezo huo umekuwa wa kujifua kwa michuano ya CHAN nchini Moroko na siku ya kesho Amavubi watacheza na Namibia kisha Jumatano wakacheza na Algeria.

Amavubi wamepangwa kundi C pamoja na Nigeria, Equatorial Guinea na Libya.

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine