RUHAGOYACU.com

Kocha wa Rwanda ataja wachezaji 17 kuwania tikiti kombe la dunia kikapu

Kocha wa timu ya Rwanda ya mchezo wa kikapu Moise Mutokambali ameweka hadharani kikosi cha wachezaji 17 ambao atawatumia katika michuano ya kuwania tikiti ya kombe la dunia.

Rwanda ilipangwa kundi B pamoja na Uganda, Mali na Nigeria.

Katika mchezo wa kwanza, Rwanda itacheza na Mali tarehe za 23-25 Februari mwaka huu.

Kikosi hicho cha Rwanda kinaanza mazoezi leo saa kumi na mbili kasorobo kwenye uwanja wa Amahoro.

Hawa wachezaji 17 wa kikosi cha Amavubi:
Mugabe Aristide (Patriots), Kubwimana Kazingufu Ali (REG), Sagamba Sedar (Patriots), Nkurunziza Walter (REG), Irutingabo Fiston (IPRC Kigali), Ndizeye Dieudonne (Patriots), Hagumintwari Steven (Patriots), Amani Deo (UGB), Nyamwasa Bruno (IPRC Kigali), Mutabaruka Victor (IPRC Kigali), Niyonkuru Pascal (Espoir ), Ruzigande Ali (APR), Niyonsaba Bienvenue (IPRC South), Shyaka Olivier (REG), Ndoli Jean Paul (IPRC Kigali), Kaje Elie (REG), Kami Kabange Milambwe (REG)

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine