RUHAGOYACU.com

Kocha Bitok aita 22 timu ya Rwanda ya mpira wa wavu

Kocha wa timu ya kitaifa ya voliboli Rwanda Paul Bitok ameita wachezaji 22 kwa ajili ya kujinoa kushiriki michuano ya mataifa ya Kombe la Mataifa ya Afrika FIVB 2018 nchini Misri.

Michuano hiyo ya wanaume itatokea tangu tarehe 20 hadi 30 Oktoba mwaka huu.
Wachezaji walioitwa wataanza mazoezi leo na wiki ijayo waingie kambini yenyewe.

Inatarajiwa kwamba kocha Bitok katikati ya mwezi ujao Oktoba atatangaza orodha rasmi ya wachezaji atakaowatumia kwenye michuano hiyo.

Rwanda ilipata tikiti baada ya kuibuka washindi katika michuano ya FIVB-Africa Zone V ikishika nafasi ya pili ikitanguliwa na Kenya.

Pia, timu ya Rwanda ilishindia medali ya Silver baada ya kushindwa na Kenya seti 3 kwa 1.

Wachezaji walioitwa:
Libero: Silvestre Ndayisaba, Bosco Mutabazi and Simon Rwigema
Setters: Jacob Cyusa, Yvan Mahoro and Jean Paul Sibomana
Kati: Madison Placide Sibomana, Ronald, Muvara, Fred Musoni, Robert Nshimiyimana, John Nkurunziza, Prince Kanamugire and Peace Twagirayesu
Kulia: Olivier Ntagengwa Olivier, Ndamukunda Flavien Christophe Mukunzi, Patrick Kavalo, Yves Mutabazi and Aimable Mutuyimana
Kushoto: Yakan Guma, Nelson Murangwa and Samuel Nyogisubizo.

Map : Nyumbani  \  Mchezo wa wavu

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine