RUHAGOYACU.com

Mpira wa wavu: APR yawasajili wachezaji wawili

Wabingwa watetezi wa ligi kuu ya wavu kwa wanawake APR imesajili wachezaji wawili kwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.

Wachezaji hao ni Benita Mukandayisenga na Flavia Dusabe kutoka Shule ya Mtakatifu Aloys.

Ligi kuu ya wavu kwa wanaume inatarajiwa kuanza Januari 13 mwaka ujao huku ligi ya wanawake ikianza mwezi wa Februari.

Mwaka huu klabu ya APR imemsajili tena Lea Uwimbabazi kutoka Sekondari ya Indangaburezi.

Timu hiyo imetwaa mataji ya ligi kuu kwa mara saba 2010, 2012, 2013, 2014, 2015, 2016 na 2017.

Map : Nyumbani  \  Mchezo wa wavu

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine