RUHAGOYACU.com

Mpira wa wavu: Gisagara yajiandaa kwa mashindano ya kimataifa Afrika, yawasajili wachezaji hawa

Kocha mkuu wa timu ya mpira wa wavu ya Gisagara Fidele Nyirimana ametangaza kuwa timu yake imejiandaa vema kwa mashindano ya kimataifa ya mpira wa wavu Afrika yanayotarajiwa kuanza Januari 13, 2017.

Kocha huyo ameambia gazeti la Ruhagoyacu kuwa wamewasajili wachezaji watatu.

" Tumesajili wachezaji ambao watatusaidia kwa mashindano ya kimataifa Afrika na katika mashindano mengine," ametangaza.

Wachezaji ambao walisajiliwa ni Nelson Murangwa kutoka Tricolorul LMV Ploiesti ya Romania kwa mkataba wa mwaka mmoja, Bob Ongom kutoka Sports S ya Uganda na Nicolas Matui kutoka Water Club kwa miktaba ya miaka miwili kwa kila mmoja wao.

Licha ya hao, timu hiyo iliwasajili wachezaji wengine kama Vincent Gasongo Dusabimana, Eugene Tuyishimire kutoka chuo cha Kibungo (UNIK) na Peter Bigirimana kutoka Rwanda Energy Group (REG).

Msimu huu, timu hiyo imewaacha Pierre Marshall Kwizera na Flavier Ndamukunda walioelekea REG na Kavalo Akumuntu aliyeshiriki UTB.

Map : Nyumbani  \  Mchezo wa wavu

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine