RUHAGOYACU.com

APR FC yakanusha madai ya kumwinda kocha mpya

Uongozi wa klabu ya APR Fc umekanusha taarifa zilizosambaa kuhusu uindaji wa kocha muu mpya kutoka Cameroon ambaye atakuwa mbadala wa Jimmy Mulisa.

Taarifa zilizofikia gazeti hili zilieleza kuwa klabu hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kumasjili kocha mkuu anayetarajiwa kupewa mikoba ya klabu hiyo mwezi huu ambapo ligi kuu itakuwa imerejea.

Minong’ono ya kubadilishwa kwake ilikazwa baada ya kumaliza mkataba wake na kukosa kuongeza mwingine huku mingine ikisema kuwa kocha huyo Mulisa aliyewahi kuwa mshambuliaji wa APR FC amepata kibarua katika Shirikisho la Soka Rwanda (Ferwafa).

Kwa mujibu wa Msemaji wa APR FC Adolphe Camarade, ameambia gazeti hili kuwa taarifa hizo ni uongo mtupu.

" Hatuna mazungumzo na kocha yeyote hata na Mkameruni huyo. Huo uongo mtupu," Camarade amefafanua.

JPEG - 170.8 kb
Hadi sasa APR Fc wanasimama nafasi ya tatu ligi kuu

Mulisa alishika usukani wa APR FC mwezi wa Novemba mwaka jana akitoka kuwa msaidizi wa mkuu wake Yves Rwasamanzi.

Licha ya kocha huyo, APR FC inaripotiwa kumsajili kiungo wa Gor Mahia ya Kenya Jean Baptiste Mugiraneza kwa ajili ya kuboresha kikosi chake baada ya kuwa nafasi ya tatu ligi na alama 17. Kwa sasa, wanata kukwea kileleni.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Daraja la kwanza

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine