RUHAGOYACU.com

Crespo kuachana na Kiyovu Sports kwa utovu wa nidhamu

Mshambuliaji wa timu ya Kiyovu Sports Sebanani Emmanuel maarufu Crespo anatarajiwa kuachana na timu hiyo mwezi huu kutokana na makosa ya utovu wa nidhami.

Taarifa kutoka chanzo cha ndani cha klabu ya Kiyovu Sports zinaeleza kuwa hana maelewano mazuri na kocha wake mkuu Cassa Mbungo hadi kumsimamisha kushiriki mazoezi ya kikosi chake.

Inadaiwa kuwa Crespo ataeleka Miroplast FC kisha Kiyovu Sports ilipe Rwf 1,500,000 kwa ziada ili ipata mshambuliaji Akffo Mohamed kutoka Ghana.

JPEG - 156.1 kb
Mshambuliaji Akffo Mohamed alisaidia Miroplast FC kusawazisha na kutoka sare ya 1-1 na Rayon Sports

Kocha Cassa Mbungo ametangaza kuwa shuruti aimarishe safu yake ya ushambuliaji.

"Tunataka kuboresha kikosi chetu ili tuendelee kubaki kileleni ligi kuu," kocha mbungo atangaza.

Tangu atoke AS Kigali bado hajashinda bao moja.

Crespo yuko baadhi ya wachezaji waliochezea timu nyingi nchini Rwanda kama Musanze FC, APR FC, Mukura Victory Sports, Police FC na Kiyovu Sports.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Daraja la kwanza

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine