RUHAGOYACU.com

Hussein Tchabalala kutua Rayon Sports kwa Rwf milioni 5

Hussein Tchabalala ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Amagaju Fc iliopo jimbo la kusini anatarajiwa kutua Rayon Sports kwa Rwf milioni 5.

Taarifa kutoka chanzo cha ndani Rayon Sports zinasema kuwa klabu hiyo itampa mkataba wa miaka miwili huku Amagaju Fc wakachukua Gilbert Mugisha kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Tchabalala , raia wa Burundi, atashirikiana na Mmali Diarra Ismaila katika safu ya ulinzi.

Naye Diarra amekuwa mali halali ya Rayon Sports mwezi huu baada ya kutoka klabu ya Darling Club Mutema Pembe ya Kongo, Jamhuriya Kidemokrasia.

Kocha mkuu wa Rayon Sports Olivier Karekezi alitaarifu uongozi wake analenga kukiboresha kikosi chake akiwasajili wachezaji watatu kwa kujiandaa imara kwa mashindano ya mabingwa Afrika ambapo ataanza akichuana na Lydia Ludic ya Burundi.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Daraja la kwanza

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine