RUHAGOYACU.com

Kocha wa Espoir FC Jimmy Ndizeye asimamishwa

Klabu ya Espoir FC imemsimasha kocha wake Jimmy Ndizeye kutokana na matokea mabaye katika ligi kuu.

Akizungumza na gazeti hili, kiongozi wa klabu hiyo Marcel Bizimana ametangaza kuwa kocha huyo amesimamishwa kwa muda.

"Tutazungumza naye kwa kujadiliana kuhusu majukumu fulani. Kwa hivo kamati ya viongozi imechukua uamuzi wa kumsimamisha," Bizimana ametangaza.

Kocha Ndizeye amesamishwa kufunza michezo miwili ijayo ligi kuu na kwa hivo usukani wake utashikwa na naibu wake Francois Kalisa.

Msimu uliopita Ndayizeye aliisaidia Espoir Fc kutinga nusu fainali ya kombe la Amani (Amahoro) baada ya kuibandua Rayon Sports.

Matokeo hayo mazuri yalifanya uongozi wa klabu yake kumuongezea mkataba.

Kwa sasa, Espoir Fc inashika mkia wa ligi kuu ikiwa nafasi ya 16 na alama 8.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Daraja la kwanza

Maoni

 1. Edward

  Tarehe 12-01-2018 saa 09:39'

  Mwandishi umekoseya unaweza kusawazisha jina la kiongozi ya kalabu ya Espoir f.c si Bizimana ila jina lake ni Habyarimana Marcel.

  Muwe na siku njema.


 • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
  Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
  Shukruni!

Habari nyingine