RUHAGOYACU.com

Aliacha Rayon Sports kuelekea APR FC: Jannot Witakenge apewa mkataba wa kuwa kocha msaidizi wa Rayon Sports

Kiungo wa zamani wa watani wa jadi nchi Rwanda Rayon Sports na APR FC Jannot Witakenge amepewa mkataba wa kuwa kocha msaidizi wa Rayon Sports akiwa mbadala wa hayati Hamad Ndikumana ’Katauti’.

JPEG - 55.3 kb
Witakenge alianza mazungumzo na Rayon Sports alipokuja Rwanda kwa mazishi ya hayati Hamad Ndikumana ’Katauti’

Mkongo huyo Witakenge ,mwenye umri wa miaka 48 kwa sasa, alitua Rayon Sports mwaka 1990 na kuwaacha akielekea St Eloi Lupopo nchini Kongo Jamhuri ya Kidemokrasia kisha akarejea Rwanda mwaka 2006 katika klabu ya APR FC dili ambayo iliwafanya mashabiki wa Rayon Sports kumchukua kama msaliti.

JPEG - 116.5 kb
Witakenge na wachezaji wa APR FC beki Mbuyu Twite na kiungo Haruna Niyonzima

Nao viongozi wa Rayon Sports walianza kuzungumza naye wakati alikuja Rwanda kwa mazishi ya hayati Hamad Ndikumana ’Katauti’ ambaye alifariki dunia kwa ghafla mwaka jana 2017 tarehe 15 Novemba.

Kabla kujiunga na Rayon Sports Jannot Witakenge alikuwa kocha mkuu wa timu ya AS Muungano jijini Bukavu ambapo alitupiwa virago mwaka jana.

Hizi timu ambazo Witakenge alizichezea:
1990-1994: Rayon Sports
1994-1996: Associacion Sportif Inter Stars
1996-1999: Rayon Sports

Mwaka elfu 2001 alikwenda na timu ya Rwanda ’Amavubi’ Ubeljiji ambapo alitoroka na kukosekana kisha akarejea tena Rwanda mnamo 2001 katika Rayon Sports kwa muda wa mwaka mmoja.

2001-2006: St Eloi Lupopo
2006-2009: APR FC

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine