RUHAGOYACU.com

Beki wa Bugesera FC Moussa Omar aelekea Sofapaka kwa Frw milioni 12,750,000

Timu ya Sofapaka ya Kenya imemsajili Beki wa Bugesera FC Moussa Omar kwa kitita cha Frw milioni 12,750,000.

Sofapaka waligundua vigezo vya ubora vya beki Mussa Omar katika Chalenji alipokuwa anaichezea timu yake ya taifa ya Burundi ’Intamba mu rugamba’.

JPEG - 91.9 kb
Beki Omar Mussa

Kiongozi wa timu ya Bugesera Jean Claude Gahigi ametangaza kuwa dili ya usajili wake imeshaafikiwa.

"Tulimalizana kila kitu na kinachobaki ni kutoa malipo," Gahigi ameeleza.

Kiongozi huyo amefafanua kuwa mchezaji huyo alisajiwa kwa dola elfu 15 sawa na 12,750,000.

Bugesera wanatarajiwa kumsajili mshambuliaji kutoka Nigeria Rafael atakayeshirikiana na Samson Ikechukwu.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine