RUHAGOYACU.com

DCMP yamuachia huru mshambuliaji Ismaila Diarra, sasa ni mali rasmi ya Rayon Sports

Timu ya Darling Club Motema Pembe nchini Kongo Jamhuri ya Kidemokrasia imempatia kibali cha kuihama (release letter) mshambuliaji Ismaila Diarra na kwa sasa ni mali ya Rayon Sports.

Ilikuwaje?
Mwaka huu mchezaji huyo alijiunga na Rayon Sports akitoka DCMP dili ambayo timu hiyo DCMP iliilaumu kuwa kinyume na sheria huku ikiidai Rayon Sports kuilipa dola elfu 14.

Hapo, mwanzoni mwa ligi kuu, Shirikisho la Soka Rwanda lilimsimamisha mchezo huyo kutokana na ukosefu wa kibali cha kuihama (release letter) timu yake ya zamani DCMP akielekea timu ya Rayon Sports.

Kesi hiyo ilimfanya mchezaji huyo kusalia nje ya uwanja miezi sita mpaka leo ambapo amepokea kibali hicho.

Katika Rayon Sports Diarra alipewa mkataba wa miaka miwili na alilipwa dola elfu 4 za kusaini mkataba wake.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine