RUHAGOYACU.com

FIFA yamruhusu mshambuliaji Ismailla Diarra kuchezea Rayon Sports

Shirikisho la Kandanda duniani FIFA limemruhusu Mmali Ismaila Diarra kuchezea timu ya Rayon Sports baada ya kujiunga na timu hiyo kinyume na sheria.

Mwaka jana Diarra alitoka Darling Club Motema Pembe (DCMP) nchini Kongo Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo na kujiunga na Rayon Sports ila DCMP ilimnyima barua ya kuihama (release letter) huku ikidai Rayon Sports kuilipa dola elfu 14.

Tatizo hilo lilifanya Shirikisho la Soka Rwanda Ferwafa kumsimamisha kwa kuvunja sheria na kuagiza timu mbili kutatua tatizo hilo.

Baada ya miezi sita bila kucheza, Diarra alipata barua ya kuihama DCMP wiki jana baada ya tatizo hilo kutatulika.

Siku ya Jumamosi, Shirikisho la Soka duniani (FIFA) ruksa ya kuchezea Rayon Sports.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine