RUHAGOYACU.com

Hatimaye mshambuliaji Savio Nshuti kuwa mali ya APR FC kwa Rwf milioni 16

Baada ya kutangaza kuvunja mkataba wake na AS Kigali mwezi uliopita, mshambuliaji Savio Nshuti yuko karibu kujiunga na APR FC.

Taarifa kufikia gazeti hili zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo ameshamaliza mazungumzo na APR FC kisiri kwa kitita cha fedha Rwf milioni 16 ingawa muda wa mkataba wake haujawekwa hadharani.

JPEG - 605.4 kb
Savio ametangaza kuwa ameachana na AS Kigali

Akizungumza na gazeti hili akiwa nchini Moroko Jijini Tanger kwa kutumikia timu ya taifa ya Rwanda Amavubi katika mashindano ya CHAN savio amefunguka kuwa aliachana na AS Kigali.

" Nikirejea sitachezea AS Kigali. Bado sijazungumza na timu yoyote ila ninachokijua ni kwamba niliachana na AS Kigali," Savio ametangaza.

Savio alijiunga na AS Kigali akitoka Rayon Sports kuelekea msimu wa 2017-2018.

Kuhusu uvunjaji wa mkataba wake inaripotiwa kuwa AS Kigali walishindwa kutimiza ahadi zao katika mkataba huo ikiwemo kumnunulia nyumba pamoja na gari.

JPEG - 91.6 kb
AS Kigali wiki iliyopita walimsainisha Mrundi Fuad Ndayisenga kwa mkataba wa miaka miwili kama mbadala wa Savio Nshuti

Nao AS Kigali wiki iliyopita walimsainisha Mrundi Fuad Ndayisenga kwa mkataba wa miaka miwili kama mbadala wa Savio Nshuti na wachambuzi wa soka wakiona dili hiyo kama ishara ya Savio kuachana nao.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine