RUHAGOYACU.com

Je, Okoko Godefroid atapewa mikoba Bugesera FC?

Viongozi wa timu ya Bugesera Fc wametangaza kuwa wameanza mazungumzo na kocha mkuu wa Gicumbi FC Okoko Godefroid kwa ajili ya kuwa mbadala wa Ally Bizimungu ambaye alitimuliwa kutokana na matokea mabaya ligi kuu.

JPEG - 322.4 kb
Kocha mkuu wa Gicumbi FC Okoko Godefroid

Kiongozi wa timu ya Bugesera FC Jean Claude Gahigi ameambia gazeti hili kuwa wamo mbioni kumtafuta kocha mpya kwani kocha wa sasa Maurice Nshimiyimana maarufu Maso amekuwa na majukumu ya kuifunza timu hiyo hadi mwisho wa mzunguko wa kwanza ligi kuu.

" Tumeanza mazungumzo na makocha wengi na mmoja wao ni Okoko Godefroid. Kocha mpya ataanza kazi yake ligi kuu ikirejea," Kiongozi wa Bugesera FC ametangaza.

Katika timu ya Gicumbi FC, kocha mkuu Okoko katika michezo 10 , alishinda 3, akashindwa 6 na kutoka sare mchezo 1.

JPEG - 156.7 kb
Kocha Ally Bizimungu alitimuliwa kutokana na matokeo mabaya ligi kuu

Okoko aliwahi kufunza timu mbalimbali nchini Rwanda Kibuye FC, Kiyovu Sports , Mukura VS, AS Muhanga, La Jeunesse na kama Gicumbi kwa sasa.

JPEG - 137.4 kb
Ally Bizimungu alitimuliwa baada ya Kanyankore Yaounde kutimuliwa tena bila kudumu

Naye Ally Bizimungu alitupiwa virago vyake akiwa mbadala wa Mrundi Gilbert Kanyankole Yaounde ambaye naye alitimuliwa bila kudumu.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine