RUHAGOYACU.com

Kocha wa zamani wa Rayon Sports Thierry Hitimana apewa kibarua Bugesera FC

Kocha wa zamani wa Rayon Sports Thierry Hitimana amepewa kibarua cha kuifunza Bugesera FC iliopo jimbo la mashariki mwa Rwanda.

" Baada ya kufanya mazungumzo na makocha wengi, mwishoni tumemteua Thiery Hitimana kushika usukani wa timu na ataanza kazi zake siku ya Jumatatu wiki ijayo," uongozi wa timu ya Bugesera FC umetangaza.

Thierry Hitimana aliwahi kuifunza Rayon Sports baada ya Mfaransa Didier Gomez Da Rosa kuachia ngazi.

Hitimana tena aliwahi kuzifunza Musanze FC na AS Kigali.

Katika Bugesera FC Hitimana atakuwa mbadala wa kocha Maurice Nshimiyimana maarufu Maso aliyepewa mikoba ya timu hiyo kwa muda baada ya kutupiwa virago kwa kocha Ally Bizimungu kutokana na matokeo.

Kocha huyo yuko baadhi ya makocha wachache nchini Rwanda walio na leseni A.

Hadi sasa, Bugesera FC wapo nafasi ya 11 na alama 11 katika michezo 11.

Habari kutoka timu hiyo zinaeleza kuwa tomu hiyo imemuongezea mktaba staa wake kama Samson Ikechukwu.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine