RUHAGOYACU.com

Migi afunguka makubwa kukataa dili ya Singida United kwa kurejea APR FC

Kiungo wa zamani wa Azam FC nchini Tanzania na Gor Mahia nchini Kenya Jean Baptise Mugiraneza maarufu Migi amefunguka makubwa kuhusu kukataa dili ya Singida United na kuchagua kurejea APR FC kwa mkataba wa miaka miwili.

"Singida United walizungumza nami wakitaka niwachezee ila niliwaambia kuwa APR FC ilishanipatia mkataba,"

" Tuliamua kuwa dili ya kuwachezea angalau inawezekana mwaka ujao," Migi ametangaza.

JPEG - 154.1 kb
Migi na mwenzake Jean Claude Iranzi ambaye alirejea APR FC akitoka Zesco United ya Zambia wakiwa mazoezini APR FC

Kiungo huyo alitoka APR FC kujiunga na Azam FC nchini Tanzania na kutoka hapo akielekea Gor Mahia ya Kenya ambapo hakuwa na maelewano mazuri na makocha wa timu hiyo.

" Walikuwa wananiweka kwenye nambari 7 au 11 kitu ambacho sikupenda kwani tangu nianze soka nilikuwa nacheza kwenye nambari 6. Hilo tatizo kubwa kwangu," amefafanua.

Kiungo huyo ametangaza kuwa pamoja na mwenzake Jean Claude Iranzi ambaye alirejea APR FC akitoka Zesco United nchini Zambia watachangia pakubwa kwa kuipatia timu hiyo taji la ligi kuu.

Katika ligi kuu ya Rwanda ARPL APR FC wapo nafasi ya 3 na alama 17.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine