RUHAGOYACU.com

Musanze FC kuachana na nahodha wake Peter Otema kwa utovu wa nidhamu

Taarifa kutoka chanzo cha ndani Musanze Fc zinasema kuwa timu hiyo itaachana na nahodha wake Peter Otema kutokana na utovu wa nidahamu ambapo hana maelewano mazuri na mkufunzi wake Sosthene Habimana.

Mshambuliaji huyo anadaiwa kususia mazoezi ya timu yake ambapo alikwenda likizoni makwao Uganda Desemba 27, 2017 kisha akachelewa kurejea mpaka Januari 15, 2017 kinyume na wenzake waliorejea mazoezini Januari 8, 2018.

JPEG - 49.2 kb
Otema alimlaumu kocha wake Sosthene kumtendea mabaya kitu ambacho hakimfurahisha

Jambo hilo lilifanya kocha wake Habimana kumvusha unahodha wa timu hiyo huku ukichukuliwa na Imurora Japhet maarufu Drogba.

JPEG - 101.5 kb
Imurora Japhet maarufu Drogba ndiye amechukua unahodha wa Musanze FC

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Otema alimlaumu kocha huyo kumtendea mabaya kitu ambacho hakimfurahisha.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine