RUHAGOYACU.com

Mwishoni: Mshambuliaji Hussein Tchabalala atua Rayon Sports kwa Rwf milioni 5

Baada ya kutumukia timu ya Amagaju FC kwa muda mwaka mmoja na nusu, mwishoni mshambuliaji Hussein Tchabalala ametua Rayon Sports ambapo amenunuliwa Rwf milioni 5.

"Tayari Tchabalala ni mali rasmi ya Rayon Sports. Tumenunua mkataba wake wa miezi sita katika klabu ya Amagaju FC yaani mpaka mwisho wa ligi kuu,"

" Muda huo ukimaliza tutazungumza upya pamoja na timu yake ya zamani makwao Burundi kama kanuni za mkataba wake zinaagiza," uongozi wa Rayon Sports umetangaza.

JPEG - 365.3 kb
Tchabalala pamoja viongozi wa Rayon Sports

Siku ya jana Jumatano alituwa jijini Kigali kumaliza dili na viongozi wa Rayon Sports na siku ya leo Alhamisi aanatarajiwa kuanza mazoezi yake katika uwanja wa Nzove.

Mshambuliaji huyo , raia wa Burundi, mshahara wake utakuwa Rwf elfu 500 kila mwezi na amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa Rayon Sports huku Mkongo Janvier Bokungu bado akiwa anajiribiwa na kocha mkuu Olivier Karekezi.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine