RUHAGOYACU.com

Picha: APR FC wajifua kushiriki mashindano ya mashujaa

Kikosi cha timu ya APR FC kimeanza mazoezi ya kujifua kushiriki mashindano yatakayofanyika kwa ajili ya kuadhimisha siku ya mashujaa.

Mashindano hayo yataanza Januari 23, 2018.

JPEG - 531.6 kb
Kocha mkuu Jimmy Mulisa


Mazoezi hayo yalifanyika jana Jumanne katika uwanja wa Kicukiro huku yakiongozwa na kocha mkuu Jimmy Mulisa.

APR FC walikuwa nane tu kwani wenzao waliitwa Amavubi kwa ajili ya kushiriki michuano ya CHAN.

JPEG - 491.3 kb
Mshambuliaji Sekamana Maxime

Inatarajiwa kuwa katika mazoezi ya siku ya leo Jumatano kutakuwepo wachezaji wapya kama Jean Claude Iranzi, Jean Baptiste Migi.

JPEG - 706.1 kb
Nahodha Albert Ngabo

Inadaiwa kuwa APR FC ilianza mazoezi na kiungo Savio Nshuti na Mghana mmoja na kinachobaki ni kumaliza dili.

JPEG - 78 kb
Nkinzingabo Fiston

Katika mashindano ya mashujaa APR FC watachuana na AS Kigali, Police FC na Rayon Sports.

Bonyeza hapa uangalie picha za mazoezi ya APR FC kwenye mtandao wa Flickr

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine