RUHAGOYACU.com

Picha: APR FC yafanya mazoezi leo, wachezaji wapya ndani

Siku ya leo Jumatatu majira ya saa nne asubuhi, kikosi cha APR FC kimeendelea kujifua kushiriki mashindano ya kuadhimisha siku ya mashujaa.

JPEG - 134.1 kb
Kikosi cha APR FC mazoezini

Katika mazoezi hayo kumeonekana wachezaji wapya ambao watatumikia timu hiyo kusaka kombe la mashindano ya mashujaa hata na taji la ligi kuu ambalo waliwahi kulitwaa mwaka 2016.

JPEG - 97.6 kb
Kiungo Jean Baptiste Mugiraneza maarufu Migi

Wachezaji hao wapya ni kiungo Jean Baptiste Mugiraneza maarufu Migi ambaye aliwahi kuichezea kabla kuelekea Azam Fc nchini Tanzania na Gor Mahia nchini Kenya ambako alitoka kurejea APR FC.

JPEG - 71.9 kb
Mshambuliaji Jean Claude Iranzi ambaye alirejea akitoka Zesco United
JPEG - 125.2 kb
Mshambuliaji Lague Byiringiro

Wengine ni mshambuliaji Jean Claude Iranzi ambaye alirejea akitoka Zesco United nchini Zambia na mshambuliaji Lague Byiringiro ambaye alitolewa katika timu ya APR FC vipukizi inayojulikana kwa jina la ’Intare FC’.

Bofya hapa uangalie picha nyingi nyinginezo za mazoezi ya APR FC.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine