RUHAGOYACU.com

Picha: Mashabiki wa Rayon Sports wamkaribisha kibabe mshambuliaji Tchabalala

Siku ya jana Alhamisi mashabiki wa Rayon Sports walimkaribisha mshambuliaji mpya Hussein Tchabalala ambaye alisajiliwa kwa Rwf milioni 5 akitoka timu ya Amagaju FC iliopo jimbo la kusini mwa Rwanda.

JPEG - 161.3 kb
Tchabalala akifika kwenye uwanja wa mazoezi wa Nzove
JPEG - 215.5 kb
Mashabiki wa Rayon Sports walimkumbatia

Mrundi huyo Tchabalala alitua siku ya jana kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu ya Rayon Sports ya Nzove ambapo timu hiyo ilikuwa inajifu kushiriki mashindano ya mashujaa na ligi kuu.

JPEG - 131.3 kb
Mashabiki walimkaribisha kibabe

Alitangaza hiki:
" Nimechagua kujiunga na Rayon Sports badala ya Kiyovu Sports kwa sababu ni timu iliyo na mashabiki wengi na kila mchezaji wake anajulikana kwa urahisi. Tena, ni timu inayotwaa makombe," Tchabalala alifunguka.

JPEG - 115.3 kb
Mazoezi ya Rayon Sports yalikuwa ya nguvu sana kila mchezaji aking’ang’ania kutafuta nafasi uwanjani

Habari kutoka chanzo cha ndani Rayon Sports zinaeleza kuwa atakuwa mbadala wa Mmali Tidiane Kone atakaelekea Musanze FC kwa mkopo.

Bonyeza hapa ungalie picha nyingi nyinginezo za ujio wa Tchabalala kwenye mtandao wa Flickr

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine