RUHAGOYACU.com

Rayon Sports yaifunga Etincelles FC 1-0 katika mchezo wa kirafiki

Wabingwa watetezi wa ligi kuu Rwanda Rayon Sports wameipiga Etincelles bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki kwenye uwanja wa Kigali.

Mchezo huo ulifanyika siku ya jana Jumatano majira ya kumi na mbili.

JPEG - 123.4 kb
Beki Eric Irambona akimtoka mchezaji wa Etincelles

Bao la Rayon Sports liliandikwa na kiungo Pierrot Kwizera dakika ya 65.

JPEG - 90.1 kb
Kocha Olivier Karekezi akimkumbatia kiungo Pierrot Kwizera baada ya kufunga bao la ushindi

Mchezo huo ulikuwa fursa ya majaribio kwa wachezaji wapya kama mshambuliaji Chris Mbondi na kiungo Jamal Mwiseneza huku tena wakijiandaa kwa mashindano ya kuadhimisha siku ya mashujaa ila washambuliaji Yassin Mugume na Hussein Tchabalala hawakucheza.

JPEG - 86.3 kb
Mshambuliaji mpya Chris Mbondi
JPEG - 104 kb
Winga Djamal Mwiseneza
JPEG - 138.5 kb
Kikosi cha Rayon Sports

Walioanza kwa Rayon Sports: Ndayisenga Kassim, Nyandwi Saddam, Irambona Eric, Mutsinzi Ange, Mugabo Gabriel, Kwizera Pierrot, Mugisha Gilbert, Nahimana Shassir, Ismaila Diarra, Chris Mbondi, Bimenyimana Bonfils Caleb

Kocha: Olivier Karekezi

JPEG - 120.9 kb
Kikosi cha Etincelles FC

Walioanza kwa Etincelles FC: Rukundo Protegene, Nsengiyumva Irshad, Niyonkuru Sadjati, Akayezu Jean Bosco, Mbonyingabo Regis, Djumapili Iddy, Mugenzi Cedrick, Akimana Tresor, Nshimiyimana Abdou, Joachim Kaliba, Muganza Isaac

Kocha: Emmanuel Ruremesha

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine