RUHAGOYACU.com

Safu ya ulinzi Rayon Sports imara: Kocha Olivier Karekezi amleta Yassin Mugume kutoka Police FC ya Uganda

Baada ya kulaumu safu yake ya ulinzi kuwa na ukame wa mabao, kocha mkuu Olivier Karekezi analenga kuimarisha safu ya ulinzi ya Rayon Sports.

Mwaka huu kocha huyo ameleta washambuliaji watatu Hussein Tchabalala kutoka Amagaju FC, Chris Mbondi kutoka Olimpia de Itá nchini Paraguay na hatimaye Mganda Yassin Mugume kutoka Police FC nchini Uganda.

JPEG - 126.9 kb
Mugume ameridhisha kocha Olivier Karekezi

Ijapokuwa kiasi cha fedha za kumsajili Mugume hakijawekwa wazi, inadaiwa kuwa Mugume amepewa mkataba wa miezi sita hadi mwisho wa mzunguko wa pili ligi kuu huku ikitarajiwa kumuongezea mkataba kutokana na hapo matokeo yake.

JPEG - 111 kb
Yassin Mugumu pamoja na kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili katika Rayon Sports Marcel Romami

Tena kocha huyo ametaarifu viongozi wake kumpa mkataba winga wa zamani wa Rayon Sports Djamal Mwiseneza ambaye alirejeshwa kwa majaribio.

Siku ya Jumatatu, Shirikisho la Soka duniani FIFA lilimruhusu Yassin Mugume kuichezea Rayon Sports kirasmi.

JPEG - 55.5 kb
Shirikisho la Soka duniani FIFA lilimruhusu Yassin Mugume kuichezea Rayon Sports kirasmi.

Wabingwa hao wa ligi kuu Rwanda watashiriki mashindano ya mabingwa barani Afrika ambapo wanatarajia kucheza na Lydia Ludic kutoka Burundi.

Map : Nyumbani  \  Rwanda  \  Habari za motomoto

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine