RUHAGOYACU.com RUHAGOYACU kuri Youtube RUHAGOYACU kuri Twitter RUHAGOYACU kuri Facebook
Habari za motomoto Yanditswe kuya 18-01-2018 saa 18:56'  -  Hii ratiba ya michuano ya mashindano ya mashujaa  |  Yanditswe kuya 18-01-2018 saa 18:14'  -  Rayon Sports yaifunga Etincelles FC 1-0 katika mchezo wa kirafiki  |  Yanditswe kuya 17-01-2018 saa 21:45'  -  Hatimaye mshambuliaji Savio Nshuti kuwa mali ya APR FC kwa Rwf milioni 16  |  Yanditswe kuya 17-01-2018 saa 17:56'  -  Migi afunguka makubwa kukataa dili ya Singida United kwa kurejea APR FC  |  Yanditswe kuya 17-01-2018 saa 17:43'  -  Safu ya ulinzi Rayon Sports imara: Kocha Olivier Karekezi amleta Yassin Mugume kutoka Police FC ya Uganda
Text Size

Chimbuko

RuagoYacu ilianzishwa na Urukundo Eric aliyeaga dunia tarehe 24 Septemba 2011 kwa ajili ya ugonjwa.

RuhagoYacu ni mradi ulionza ukiwa blogu kwa lengo la kutangaza habari moto moto za uhondo kwa mashabiki wa soka nchini Rwanda na Wanyarwanda kwa ujumla.

Blogu hiyo baada ya muda ilipokelewa vema na kupendwa sana kwa hivo kukaibuka pendekezo la kuibadilisha iwe tovuti kwa sababu ya habari nyingi zilizokuwa zimeshapatikana na shuruti zipashwe Wanywarwanda na wengi wengineo katika pande tofauti za dunia.

Sababu kuleta jina la RuhagoYacu

Sababu kuleta jina RuhagoYacu ni kwamba katika lugha ya Kinyarwanda, jambo Ruhago linabeba maana ya ’mpira’ au ’kabumbu’ na jingine la ziada Yacu likabeba maana ya ’yetu’. Kwa hivo, kulikuwa na wazo la kuwahimiza Wanyarwanda wapende uchezaji wa soka na vile kuufanya uwe kama utamaduni wao.

Lengo

Lengo la RuhagoYacu ni kupasha Wanyarwanda habari moto moto, mpya na pia za ushahidi na uhakika kuhusu soka pamoja na michezo mingine. Habari hizo zikatangazwa katika lugha tatu zilizo Kinyarwanda, Kiingereza na Kiswahili.

Licha ya hayo, si chombo cha habari tu ila pia kuna kipindi cha maoni ya waeledi waliwo na uzoefu na tajribu kuhusu soka nchini Rwanda na kwingineko duniani.

Hapo, RuhagoYacu itakuwa muungano wa Wanyarwanda kuleta maoni yao kwa kuinua kiwango au kuchangia kuendeleza soka nchini Rwanda pamoja na michezo mingine.

ABAYOBOZI BAKURU