RUHAGOYACU.com
RuhagoYacu  |  Ulaya  |  Ligi

Arsene Wenger ashtakiwa na FA kutokana na tamko lake kuhusu mwamuzi Mike Dean

Mwalimu wa timu ya Arsenal Arsene Wenger amefunguluwia amshtaka na Chama cha Soka England (FA) kutokana na tamko lake kuhusu waamuzi.

Wenger alifanya hivo baada ya timu yake ugenini Jumapili kulazimishwa sare ya 1-1 na West Brom kisha akikasirikia mwamuzi Mike Dean kwa kuwapa West Brom mkwaju wa penalti ulifungwa na kuwafanya kusawazisha huku mechi ikisalia dakika moja kumalizika ambapo Calum Chambers aliadhibiwa baada ya Kieran Gibbs kuusukuma mpira na ukagusa mkono wake.

Wenger alihisi kwamba mchezaji huyo hakuunawa mpira huo makusudi.

Baada ya mechi kumalizika, Wenger anadaiwa kuingia chumba cha kubadilishia mavazi cha waamuzi na kubwaga matusi ya kukera huku akitilia shaka uwezo Mike Dean.

Wenger amepewa hadi saa 18:00 GMT Ijumaa kujibu mashtaka hayo.

Januari, alipigwa marufuku kutokuwa uwanjani mechi nne baada ya kupatikana na hatia kumhusu mwamuzi Anthony Taylor mechi ya ligi dhidi ya Burnley.

Arsenal, walio nafasi ya tano Ligi ya Premia kwa sasa, watakutana na Chelsea walio nafasi ya tatu Jumatano (19:45 GMT- saa tano kasorobo usiku Afrika Mashariki).

Sheria za soka zinasema adhabu inafaa kutolewa tu iwapo mchezaji alinawa mpira makusudi na kwamba umbali kati ya mchezaji mpinzani na mpira unafaa kuzingatiwa.

Chanzo: BBC/Michezo/Kiswahili

Map : Nyumbani  \  Ulaya  \  Ligi

Maoni


  • MAELEKEZO KUHUSU MAANDIKO YA MAONI YAKO:
    Andika jina na barua pepe yako pahali penyewe. Maoni yako yanatolewa baada ya kukaguliwa na RuhagoYacu.com. Ikiwa maoni yako yaenda kinyume na habari zilizopo pia na kanuni za wanamichezo hapo yanafutiliwa.
    Shukruni!

Habari nyingine